You are currently viewing Kinshasa : Vital Kamerhe asimamiya kikao kipya cha bunge la taïfa wakati wanabunge kadhaa wanapanga kumutimuwa madarakani mwa kiongozi wa bunge hilo

Kinshasa : Vital Kamerhe asimamiya kikao kipya cha bunge la taïfa wakati wanabunge kadhaa wanapanga kumutimuwa madarakani mwa kiongozi wa bunge hilo

Spika wa bunge la taïfa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Vital Kamerhe, aliongoza kikao cha kwanza cha mwezi wa kenda baada ya likizo ya miezi mitatu mfululizo, siku ya kwanza tarehe 15 Mweze wa kenda, 2025. Mkutano huo ulifanyika kwenye ikulu ya bunge mkowani Lingwala mjini Kinshasa, kama ilivyo kawaida. Katika hotuba yake ya ufunguzi, Vital Kamerhe alihutubia kwa kujitambua, ingawa alisisitiza juu ya uzoefu wake wa muda mrefu katika siasa za nchi.

Hata hivyo, wabunge waliokuwa wakishinikiza kuangushwa kwake katika cheo hicho, wakiongozwa na Mbunge aliyeteuliwa kutoka mji wa Butembo, jimboni Kivu ya Kaskazini, Crispin Mbindule Mitono, walijumuisha waraka wenye saini za zaidi ya mia, wakimwonyesha spika kuwa wanataka afukuzwe bungeni.

Vital Kamerhe ni mwanasiasa mwenye historia ndefu na aliyekuwa mshirika wa karibu wa Rais wa jamhuri Felix Tshisekedi Tshilombo kabla ya kuingia madarakani. Awali alijitokeza kama msaidizi muhimu wa Rais Tshisekedi, na walipatikana kuungana kwenye mrengo wa kisiasa wa CASH, ambao baadaye ulibadilishwa na FCC-CASH na hatimaye kuwa « Union Sacrée de la Nation, » muungano wa kisiasa unaoendelea kuimarisha serikali ya sasa.

Kwa upande wake, Felix Tshisekedi, ambaye ni raisi wa sasa, anajivunia kuwa kiongozi wa kwanza wa jamhuri ya kidemocrasia ya Kongo tangu kuendelea kwa mabadiliko ya kidemokrasia kuweza kuunganisha vyama vyenye tofauti kibiashara na kisiasa chini ya umoja mmoja unaojulikana kama Union Sacrée. Hii ni sehemu ya historia ya kisiasa ya nchi inayoshuhudia mageuzi na muungano wa wenye dhamira ya kuleta utulivu na maendeleo nchini humu.

Rodrigue MUMBERE VUTALA
Mhariri

Laisser un commentaire